Maswali yaliyoulizwa mara nyingi :
Je naweza kutumia e-Mikutano
wakati wa usiku?
Ndio, mfumo wa e-Mikutano unapatikana muda wote katika siku zote za juma.
Unachotakiwa kufanya ni kupanga mapema muda wa kufanya mkutano na kisha kutuma maombi ya
kuwekewa nafasi kupitia linki iliyopo kwenye ukurasa wa kwanza wa e-mikutano.
Je naweza kuanzisha mkutano bila kuomba ruhusa au kuweka nafasi kabla?
Hapana, ni muhimu kufanya maombi ya mkutano kabla ya muda.
Inashauriwa kupanga mkutano wako mapema na kuweka nafasi kwenye mfumo
siku mbili kabla kwani waombaji ni wengi.
Je mtu yeyote anaweza tuma
maombi ya kuwekewa nafasi ya
mkutano kwenye mfumo e-
mikutano?
Hapana, mfumo huu ni kwa ajili ya Taasisi za
Umma, wanaoweza kuomba nafasi kwenye mfumo
ni Afisa TEHAMA wa taasisi husika kupitia jina na
nywila zake anazotumia kwenye mfumo wa GISP ( https://gisp.gov.go.tz/login )
Ni siku zipi au muda gani
ninaruhusiwa kuomba nafasi ya
kufanya mkutano?
Unaweza kuomba nafasi ya kufanya mkutano muda
wowote.
Nafasi utakayopewa inategemea na waombaji wengi
waliokutangulia. Mfumo unakuruhusu kuchagua siku,
muda wa kuanza mkutano na kiasi cha muda
ambacho mkutano utatumia.
Ili kufanya maombi ya nafasi ya
mkutano inanitaka niweke jina na
nywila. Je naweza kujisajili kwa
njia gani ili kupata jina na nywila
za kuingilia kwenye mfumo wa
kuombea nafasi?
Anaetakiwa kuomba nafasi ya mkutano ni afisa
TEHAMA wa Taasisi aliesajiliwa kwenye mfumo wa
GISP kwa niaba ya Taasisi husika. Jina na nywila
anayotumia kuingilia kwenye mfumo wa GISP ndio
zinatumika kuingilia kwenye mfumo wa kuombea
nafasi za mkutano.
Nimeshindwa kuipata e-Mikutano
simu App kwenye Playstore na
iStore?
App ya e-Mikutano inapatikana kwenye linki iliyopo
ukurasa wa kwanza wa tovuti ya e-Mikutano.
Gonga linki hiyo na kisha pakua mfumo.
Mbona e-Mikutano App haikubali
kusakinisha (install) kwenye simu
yangu?
App ya e-Mikutano inatumika kwa simu za Android
tu na zenye mfumo endeshi (OS) kuanzia tolea la 7.
Mfumo wa e-Mikutano unatakaa
kuunganishwa kwenye kivinjari
changu.
Mfumo huu kwasasa unapatikana kwa kutumia kivinjari cha Google Chrome na Chromium.
Tufanyeje kuendelea na mkutano
kama tupo kwenye Mtandao usio
imara?
Inashauriwa kufifisha(mute) video kwa baadhi ya
wajumbe au wote na kuendelea na kuwasiliana kwa
sauti tu ili kuongeza ubora.
Naweza kuwaona washiriki wote
lakini wao hawanioni. Nini tatizo?
Angalia kama kamera yako imewashwa au kivinjari
chako kimeruhusu e-mikutano kutumia kamera
yako. Kama ruhusa imetolewa basi angalia kama
kamera yako haijazibwa na kitu na jaribu kukifuta.
Ni idadi ya watu wangapi nina
ruhusiwa kuwaalika kwenye
mkutano wangu?
Inaruhusiwa kualika mpaka watu 20 kwa mkutano
mmoja. Kama kuna ulazima wa kuwa na wajumbe
zaidi ya 20 kwenye mkutano unashauriwa
kuwasiliana na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa
msaada zaidi.
Nawezaje kuzuia mtu asiehusika
kuingia kwenye mkutano wetu?
Ni muhimu kutoa au kugawa namba na nywila ya
mkutano kwa wahusika kwa kutumia njia sahihi na
yenye usiri na usalama. Wahusika hawatakiwi kuitoa
namba na nywila ya mkutano kwa mtu asiyehusika pia
kabla ya muda wa mkutano kuhakikisha wanaiweka
kwenye kumbukumbu salama.
Kuna muingiliano wa sauti kati ya
mtu anaeongea na nyingine
zinazoleta kelele na kufanya
kutosikilizana vizuri. Nini kifanyike?
Inashauriwa kama mshiriki hazungumzi basi ni
muhimu azime au afifishe kinasa sauti chake. Kwani
kinasa sauti kina tabia ya kuchukua sauti za
mazingira mtu alipo na kuziingiza kwenye mfumo
hivyo kuleta mchanganyiko na sauti ya mzungumzaji
unaopelekea kuwa na kelele.