Picha haipo

Maswali yaliyoulizwa mara nyingi :

Je, kuna utofauti wowote kati ya eMikutano toleo la kwanza na toleo la pili?

Ndio, toleo la pili inakuruhusu kuomba mkutano kwa kutumia web app na simu app (mobile application)
Toleo la pili inaruhusu mtumishi yoyote mwenye barua pepe ya serikali kuomba nafasi ya mkutano.

Je, Ninaweza kuomba vikao vingapi kwa siku?

Unaruhusiwa kuomba vikao vitano kwa siku na vinaweza kufanyika kwa muda mmoja.

Je, kwanini tunaandika namba za simu?

Ili kupata taarifa fupi za Mikutano yako uombayo

Je naweza kutumia e-Mikutano wakati wa usiku?

Ndio, mfumo wa e-Mikutano unapatikana muda wote siku zote za juma. Unachotakiwa kufanya ni kupanga mapema muda wa kufanya mkutano na kisha tuma maombi ya kuwekewa nafasi kupitia linki iliyopo kwenye ukurasa wa kwanza wa e-mikutano

Je naweza kuwaalika washiriki kwenye mkutano kupitia ukurasa wa maombi kwa kutumia barua pepe zao?

Ndio, utaweza kuwaalika kwa kutumia barua pepe yoyote ya mshiriki.

Nawezaje kupata Tokeni ya mratibu?

Tokeni ya mratibu itapatikana tu kwenye akaunti yako ya maombi pale tu unapoomba mkutano ili kuzuia kupatikana kwa mtu mwingine.

Je naweza kuanzisha mkutano bila kuomba ruhusa au kuweka nafasi kabla

Hapana, ni muhimu kufanya maombi ya mkutano kabla ya muda. Unashauliwa kupanga mkutano wako mapema na kuweka nafasi kwenye mfumo siku mbili kabla kwani waombaji ni wengi.

Je mtu yeyote anaweza tuma maombi ya kuwekewa nafasi ya mkutano kwenye mfumo e- mikutano?

Hapana, mfumo huu ni kwa ajili ya Taasisi za Umma, wanaoweza kuomba nafasi kwenye mfumo ni maafisa/watumishi wa serikali kupitia barua pepe ya serikali na nywila aliyopewa anaweza kuomba nafasi ya mkutano.

Ni siku zipi au muda gani ninaruhusiwa kuomba nafasi ya kufanya mkutano?

Unaweza kuomba nafasi ya kufanya mkutano muda wowote. Mfumo unakuruhusu kuchagua siku, muda wa kuanza Mkutano, kiasi cha muda ambacho mkutano utatumia, na idadi ya Washiriki.

Ili kufanya maombi ya nafasi ya mkutano inanitaka niweke jina na nywila. Je naweza kujisajili kwa njia gani ili kupata jina na nywila za kuingilia kwenye mfumo wa kuombea nafasi?

Anaetakiwa kuomba nafasi ya mkutano ni mtu yoyote mwenye namba ya simu inayotambulika na kutumika, barua pepe ya serikali na nywila unazotumia kwenye Mfumo wa barua wa serikali (Government Mail System (GMS)).

Nimeshindwa kuipata e-Mikutano simu App kwenye Playstore na iStore?

App ya e-Mikutano inapatikana kwenye linki iliyopo ukurasa wa kwanza wa tovuti ya e-Mikutano. Gonga linki hiyo na kisha pakua mfumo.

Mbona e-Mikutano App haikubali kusakinisha (install) kwenye simu yangu?

App ya e-Mikutano inatumika kwa simu za Android tu na zenye mfumo endeshi (OS) kuanzia tolea la 7.

Mfumo wa e-Mikutano unatakaa kuunganishwa kwenye kivinjari changu.

Mfumo huu kwasasa unapatikana kwa kutumia kivinjari cha Google Chrome na Chromium.

Tufanyeje kuendelea na mkutano kama tupo kwenye Mtandao usio imara?

Inashauriwa kufifisha(mute) video kwa baadhi ya wajumbe au wote na kuendelea na kuwasiliana kwa sauti tu ili kuongeza ubora.

Naweza kuwaona washiriki wote lakini wao hawanioni.Nini tatizo?

Angalia kama kamera yako imewashwa au kivinjari chako kimeruhusu e-mikutano kutumia kamera yako. Kama ruhusa imetolewa basi angalia kama kamera yako haijazibwa na kitu na jaribu kuifuta.

Ni idadi ya watu wangapi nina ruhusiwa kuwaalika kwenye mkutano wangu?

Inaruhusiwa kualika mpaka watu 30 kwa mkutano mmoja. Kama kuna ulazima wa kuwa na wajumbe zaidi ya 30 kwenye mkutano unashauriwa kuwasiliana na dawati la msaada.

Nawezaje kuzuia mtu asiehusika kuingia kwenye mkutano wetu?

Ni kwa kumkataa mshiriki kutoka kwenye chumba cha kusubiria (lobby room). Pia ni muhimu kutoa au kugawa tokeni ya mkutano kwa wahusika kwa kutumia njia sahihi na yenye usiri na usalama.

Kuna muingiliano wa sauti kati ya mtu anaeongea na zingine zinazoleta kelele na kufanya kutosikilizana vizuri. Nini kifanyike?

Inashauri kama mshiriki hazungumzi basi ni muhimu kuzima au kufifisha kinasa sauti chake. Kwani kinasa sauti kina tabia ya kuchukua sauti za mazingira mtu alipo na kuziingiza kwenye mfumo hivyo kuleta mchanganyiko na sauti ya mzungumza unaopelekea kuwa na kelele.