Picha haipo

Kufanya na kuendesha mkutano

Jinsi ya kuomba nafasi ya mkutano

Mikutano yote kwenye mfumo wa e-Mikutano ni lazima iwe imepangwa kabla.

Bonyeza #1, kisha #Zaidi kubadili lugha. Fungua kivinjari na andika anuani ya tovuti ya mfumo: mikutano.gov.go.tz

Bonyeza #2 kwenda kwenye mfumo wa maombi ya nafasi ya kufanya mkutano.

Baada ya kubonyeza #2 utapelekwa kwenye ukurasa wa mfumo wa maombi.

#3 Jaza barua pepe ya serikali na nywila yako ya mfumo wa GMS kuingia kwenye mfumo wa maombi.

Bonyeza #4 Kufugua akaunti ya Maombi kama hautumii mfumo wa GMS.

Kumbuka ni mtumishi wa serikali tu ndio anaruhusiwa kufungua na kuomba Mkutano.

Bonyeza #5 Kama umesahau nywila ya mfumo wa maombi

#7 na #8 zitakupeleka kwenye ukurasa wa mwanzo wa nyumbani wa mfumo wa mkutano.

#9 Kwa ajili ya kufahamu maboresho yaliyofanyika katika mfumo.

Kwa mtumiaji wa mara ya kwanza mwenye GMS baada ya kujaza taarifa kwenye namba #3 utapelekwa kwenye #10 kuweka namba yako ya simu kwa ajili ya kutumiwa ujumbe mfupi wenye tokeni utaoingiza kwenye #11 ili uweze kuthibitisha na kumalizia usajili wako.

#6 Kuthibitisha na kumalizia usajili itakupeleka kwenye #11 kukamilisha usajili

Baada ya kubonyeza #5 utapelekwa kwenye ukurasa wa kuandika barua pepe yako kwaajili ya kupata nywila mpya kama inavyoonekana kwenye #12

Baada ya kubonyeza #4 jaza taarifa zako sahihi kama inavyoeleza kwenye #13

Kisha bonyeza namba #14 ili utumiwe linki ya kuhakiki kwenye barua pepe yako.Utakapo bonyeza linki uliyotumiwa itakurudisha ukarasa wa maombi kuweza kuthibitisha na kukamilisha usajili wako kwa kuingiza tokeni utayotumiwa kwa simu kwenye #15

Bonyeza #16 kuondoka kwenye kibox cha kuweka tokeni

Bonyeza #17kukamilisha usajili

Bonyeza #18 kuona vikao vitano vya tarehe ya mwanzo

Bonyeza #19 kuomba kikao

Bonyeza #20 kuona vikao vyote ulivyoomba, ulivyofanya na kufuta

Bonyeza #21 kuona vikao vyote ulivyofanya

Bonyeza #22 kuona vikao vyote ulivyofuta

Bonyeza #23 kupata msaada wa namna ya kutumia mfumo wa e-Mikutano kwa njia ya maswali

Bonyeza #24 kuanza Mkutano kama mratibu

Baada ya kubonyeza #19utaletewa ukurusa wa kujaza taarifa za Mkutano unaohitaji kuomba kama inavyoonekana kwenye #25

Bonyeza #26 kuweza kutuma taarifa za mwaliko wa mkutano kwa wahusika kwenye barua pepe na kupata majibu kupitia ukurasa wako wa Maombi.

Bonyeza #27 kutuma maombi yako ya Mkutano

Baada ya kubonyeza #27utapata ujumbe kama inavyoonekana kwenye #28

Kujiunga kwenye Mkutano kama mratibu

Baada ya kubonyeza #24 kama mratibu itakuletea kuandika jina lako kama inavyooneka kwenye #29

Bonyeza #30 kujiunga na Mkutano. Tayari utakuwa upo kwenye chumba cha Mkutano

Bonyeza #31 kukubali au #32 kukataa mshiriki

Kujiunga na Mkutano kama mtumiaji wa kawaida

Namba ya mkutano na Majina yako ni muhimu:

#33 weka tokeni ya mshiriki uliopewa na mratibu kisha bonyeza Ingia

Weka majina yako kama inavyoonyesha #29 ili uweze kutambulika na mratibu, kisha bonyeza namba #30 Kujiunga

Kisha msubirie mratibu akuruhusu

Bonyeza #34 kuweka nywila endapo utakuwa umepewa na mratibu

Bonyeza #35 kuwezesha chumba cha kusubiri

Bonyeza #36 kuweka nywila hii ni kwa upande wa mratibu tu

Bonyeza #37 kuwezesha usalama (end-to-end encryption)

Kuonesha faili au taarifa

Bonyeza #38 kuonesha faili au taarifa ambapo unaweza chagua kama ifuatavyo: a) Kuonesha skrini yako “entire screen” b) Kuonesha faili na taarifa zake. Faili lazima liwe limefunguliwa kwanza kisha bonyeza Application Window kisha chagua faili husika.

Bonyeza #39 (Mkono) kunyoosha mkono ili kuomba ruhusa ya kuongea. Nimuhimu kama huongei kuzima kinasa sauti na kukiwasha baada ya kuinua mkono.

Bonyeza #40 (Chat) kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa watu wote au mmoja mmoja.

Kwa Mpangilio zaidi

Baada ya kubonyeza #41, utaingia na kubonyeza #43 ambapo utakutana na taarifa zifuatazo:

Bonyeza #42 kwa ajili ya kuruhusu Usalama (Security Options) wa mkutano wako

Bonyeza #44 Kufungua dokumenti ya kushiriki pamoja

Bonyeza #45 “vifaa” kuchagua kifaa cha kutumia kama kinasa sauti, kamera na spika. Unaweza tumia za kwenye komputa/simu yako au vya kuweka na kutoa.

Bonyeza #46 “wasifu” kuweka jina na barua pepe yako. Jina utakalo weka hapo ndio litaonekana kila wakati unapojiunga na mkutano. Ni muhimu kuweka majina yote la kwanza na la ukoo/mzazi.

Bonyeza #47 “zaidi” kuchagua lugha. Lugha ya mfumo huu ni Kiswahili lakini unaweza chagua zingine.

Bonyeza #41 kisha #44 kufungua dokumenti itakayoruhusu kubadilisha kwa kuandikia kama inavyoonekana kwenye #48

Kufifisha sauti na video na kumaliza mkutano

Bonyeza #49 (Kinasa sauti) kufifisha sauti. Ni muhimu kufifisha muda wote ambapo huongeza kupunguza muingiliano wa sauti na mzungumzaji.

Bonyeza #50 (Kuondoka/Kutoka) kutoka kwenye mkutano.

Bonyeza #51 (Video kamera) kufifisha video. Inashauriwa kama mpo wengi na mtandao sio mzuri basi mfifishe video zenu ili kuendelea kuwasiliana kwa sauti.